Header Ads Widget

Responsive Advertisement

YANGA YACHAPWA KWA MKAPA LIGI YA MABINGWA AFRIKA


 




Klabu ya soka ya Yanga SC wameanza vibaya Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuchapwa 1-0 na Rivers United ya Nigeria katika mechi ya kwanza iliyopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.





Bao lililoizamisha Yanga limefungwa na Omoduemuke Moses dakika ya 51 akitumia udhaifu wa safu ya ulinzi ya Yanga na ufupi wa kipa wao, Djigui Diarra. 

Ili iweze kusonga mbele Yanga SC sasa watatakiwa kuupanda mlima kwenye mechi ya marudiano Septemba 19 Uwanja wa Adokiye Amiesimaka Jijini Port Harcourt, Nigeria kwa kushinda si chini ya mabao 2-0

Post a Comment

0 Comments