Baada ya wiki tano za kampeni, bunge lililochaguliwa na Wacanada wakati huu linaonekana sawa na lilie walilopigia kura mwaka t2019.
Justin Trudeau amesalia madarakani lakini anakosa wingi wa wajumbe Chama cha Conservative kimeshinda kura ya wengi lakini kimekosa viti vya kutosha kumuondoa madarakani Trudeau wa chama cha Liberal.
Ijapokuwa matokeo yataendelea kuwasilishwa katika siku zijazo wakati maafisa wa uchaguzi wanaendelea kujumuisha kura zilizopigwa kwa njia ya posta, hakuna kinachokadiriwa kubadilisha matokeo jumla ya uchaguzi.
Trudeau aliangazia hatua hiyo kama ushindi katika hotuba kwa wafuasi mapema Jumanne, akiwaambia kuwa "tulichoona usiku wa leo ni mamilioni ya Wakanada [ambao] wamechagua mpango wa maendeleo"


0 Comments