Liverpool imefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Leeds United usiku wa Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Elland Road.
Mabao ya Liverpool yamefungwa na Mohamed Salah dakika ya 20, hilo likiwa bao lake la 100 katika Ligi Kuu ya England, Fabinho dakika ya 50 na Sadio Mane dakika ya 90.
Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 10 sawa na Manchester United na Chelsea baada ya wote kucheza mechi nne sasa wakifuatana nafasi tatu za juu




0 Comments