
Hakuna siku ambayo niliumia kama siku mume wangu alipomleta mwanamke nyumbani
kwetu tunapoishi mimi na yeye, akaingia naye ndani na kufanya naye mapenzi
chumbani huku mimi nikiwa sebuleni na mtoto mdogo wa miezi tisa. Wakati huo
ndoa yetu ilikua na miezi minne, katika kipindi chote hicho cha ndoa mwanzo
tulikua vizuri, alianza kubadilika baada ya kukaa mwaka mmoja bila kupata
mtoto, sio kwamba nilikua sibebi ujauzito, hapana, nilikua nabeba sana tu
lakini mimba zilikua zikifikisha miezi minne zinaharibika.
Alianza kuchepuka akiniambia kuwa anatafuta mwanamke wa kuzaa naye, nililazimika kuvumilia kwani nilikua bado nampenda, mimi nilikua ni Mama wa nyumbani alishanikataza kufanya kazi. Alianza kubadilisha wanwake kama nguo, nilipoongea kila mtu aliniambia vumilia kwani hakuna mwanaume ambaye anaweza kukaa bila mtoto tatizo ni la kwangu. Nyumbani kwao hasa Mama yake ndiyo alikua anamsisitiza kabisa kuoa mwanamke mwingine kwani dini inaruhusu.
Hakua akitaka kuoa kwani alikua na wanawake wengi, nilifanikiwa kupata ujauzito ila kama kawaida walijua kua itatoka, lakini Mungu alijaalia nilijifungua mtoto wakiume, nikiamini kuwa atabadilika kwakua nina mtoto ndiyo mambo yalizidi kuwa mbaya. Mume wangu alipata pesa dharau ndiyo zikazidi, alijenmga nyumba nzuti tu akawa analeta wanwake ndani mimi nikiwepo. Nilikua naumia sana, kuna kipindi nilikasirika na kuamua kurudi kwetu, kipindi hicho mwanangu alikua na miezi minne.
Alikuja na kujifanya mtakatifu, akawa analalamika kuwa nimemkimbia, Baba yangu alinilazimisha kurudi kwa mume wangu. Kwakua sikua na kazi na nilikua namtegemea kwa kila kitu nililazimika kurudi kwake, baada ya kurudi alianza kulalamika kuwa nimemdhalilisha, aliacha kutoa pesa ya matumizi na kuwa ananipiga kila siku, nilikua naumia sana nateseka mtoto anateseka kwani maziwa yalikua hayatoki. Mara kibao alikua ananifungia ndani bila kunipa kitu chochote, kuna siku alinifungua ndani kwa siku mbili.
Ndani kulikua na unga tu, hakukua hata na mafuta, nililazimika kupika uji ili kunywa maziwa yatoke nimnyonyese mwanangu, wakati huo alikua na miezi saba, mtoto alikua analia sana, alikua na njaa, hakukua na kitu cha kumpa, uji ulikua haunyweki na nilijua kama tutakufa. Lakini Mungu alituponya, mume wangu alirudi akaleta chakula, alishaninyang’anya simu na alikua hataki kabisa mimi kutoka ndani kwa madai kuwa namtangaza kwa watu kuwa hahudumii. Nilivumilia, nilikua kama mfungwa kwani ukitoka nnje kila mtu ananiona kuwa mimi ndiyo mbaya.
Nilikua nimekonda sana na maneno hata ya ndugu zangu nikuwa nilikua nimekonda kwasababu nina roho mbaya. Hata Mama yangu nilipokua nikimlalamikia alikua akiniambia kuwa mimi si mvumilivu. Mwanngu akiwa na miezi tisa ndiyo siku ambayo niliumia kuliko siku nyingine zote. Mume wangu alikuja na mwanamke wake, wote walikua wamelewa, nakumbuka ilikua ni jioni, siku ya jumapili, sitaisahau hiyo siku maishani mwangu. Alinipita sebuleni na kuingia chumbani na mwanamke wake, walifanya mapenzi mimi na mwanangu tukiwa sebuleni.
Kilikua ni kama kitu cha kawaida na nilishazoea, baada ya kumaliza mambo yao walitoka na kuniacha mimi na mwangu. Ilikua ni usiku kama saa mbili hivi ndiyo walitoka, nilishapika kumuandalia chakula, kilikua mezani lakini hakula nilitakiwa kumsubiri mpaka arudi kwani nikila bila yeye basi ni vipigo. Nikiwa nimekaa sebuleni nimembeba mwanangu nilijikuta napitiwa na usingizi. Nilijkuja kuzinduka baada ya kama nusu saa hivi, naangalia pembeni mtoto simuoni, sikushtuka kwani alikua anatambaa vizuri tu na kushika vitu kusimama.
Nilinyanyuka kuanza kumtafuta huku nikimuita, sikusikia kelele zake nilienda mpaka chumbani, mlango wa chumba changu ulikua umefunguliwa nikajua lazima atakua ameingia huko. Kweli alikua kaingia, niliingia na kuwasha taa. Nlichokikuta ndiyo kilibadilisha maisha yangu mpaka hii leo. Nilimkuta mwanangu kakaa chini kashika Condom iliyotumika, zilikua kama tatu pale chini na mwanangu alikua anakula shahawa za Baba yake, aliniona na kuanza kucheka, alininyooshea kama ananipa.
Kidogo nidondoke kwani alionekana kuanza muda mrefu, kuna nyingi tu zilikua zimemwagikia mdomoni na kwenye nguo. Mara nyingi mume wangu akiingiza wanawake zake chumbani hatumii condom na ni kazi yangu kufua mashuka, anafanya hivyo makusudi tena kwa matudi akiniambia kuwa mimi ni kula kulala hivyo ndiyo kazi yangu hawezi kunilisha bure. Lakini siku hiyo sijui kwanini alifanya hivyo akatumia Condom. Nilimkimbilia mwanangu na kumnyang’anya, nilianza kumsafisha nikamuogesha na kumfuta vizuri.
Kwa namna nilivyoshtuka mwanangu alilia sana. Siku hiyo ndiyo kila kitu kilibadilika katika maisha yangu, baada ya kumuogesha mwanangu nilikusanya nguo zake, nikaweka kwenye Begi vizuri kisha nikakusanya na za kwangu. nilitoka nnje usiku uleule, nikaenda sehemu kulikua na Bajaji, nikaiita moja na kumuomba Dereva bajaji aje kunichukua. nilifunga nyumba na kuchukua funguo nikaipelekwa kwa jirani yetu mmoja, nilimuambia Dereva Bajaji tuondoke, aliniuliza tunaenda wapi nikamuambia kuwa sijui lakini tuondoke.
Nilikua nalia huku nimempakata mwanangu, njiani dereva alihisi kuwa siwezi kumlipa, alisimamisha Bajaji na kuniambia kuwa nimpe pes ayake kwanza, sikua na hata Shilingi kumi, kwa hasira alinishusha, nilijaribu kumuelezea matatizo yangu lakini aliniambia kuwa hata yeye ana yakwake hawezi kusaidia kila mtu. Alitukana sana na kuondoka kwa hasira akinicha na mwanangu. Nilimbeba mwanangu mgongoni, nikachukua mabegi yangu na kuanza kuzunguka nayo, nilikua nikitembea sijui naenda wapi, nilitembea tu kwenda mbele ili mradi kufika mbali.
Nilikua kama nimechanganyikiwa, sikutaka kwenda kwa ndugu kwani wasingenipoke ana hata kama wangenipokea basi wangempigia simu mume wangu na kumuambia na ninavyomjua angekuja tu kunichukua akijifanya hakuna kitu kilichotokea bali mimi ndiyo nakua sitaki kuishi naye. Nilitembea mpaka nikachoka, nikafika kwenye mtaro mmoja, nikarusha mabegi yangu na kulala hapohapo. Bahati nzuri mwanangu hakulia, alilala, hata hakuamka kunyonya mpaka subuhi.
Nilikua na njaa na sikua na hata Shilingi mfukoni, mtoto aliamka na kuanza kulia, nilijaribu kumnyonyesha lakini maziwa hayakutoka. Akili ilifanya kazi harakaharaka, niliangalia mbele kulikua na vibanda vingi vya Mama lishe, nilienda na kuongea na Mama mmoja nikamuomba maziwa tu nimpe mwanangu, kweli alikubali, alinipa nikampa mtoto akanywa akatulia. Nilimuomba kazi yoyote ya kufanya lakini alikua hana, na kwakua nilikua na mtoto asingeweza kunisaidia.
Akili ilifanya kazi harakaharaka, nilichukua begio yangu na kutoa baadhi ya nguo, nilimuomba yule Mama kunihifadhia mabegi mengine kisha nikaanza kuzunguka kama mmachinga, mwanangu mdgongoni nauza nguo. Sikua na nguo nzuri sana lakini niliuza, siku ile niliuza nguo za kama elfu ishirini, niliiangalia na kuiona kama mtaji, ingawa sikua na sehemu ya kulala lakini halikua jambo la muhimu sana kwa siku hiyo. Nilipata chakula na kesho yake niliendelea kuuza nguo nyingine, niliuza za kwangu na baadhi ya nguo za mtoto.
Kipindi hicho nilikua bado nalala kwenye vobaraza vya maduka, nilipata kama laki mbili, nikaenda kutafuta chumba cha elfu kumi na tano, nikalipia miezi mitatu na hapo ndiyo niakaanza maisha yangu mwenyewe. Nilununua baadhi ya vitu vya ndani kama jiko sufuri na sahani. Nikaanza kupika mandazi asubuhi na mchana nazungusha nguo za mtumba hasa za watoto. Mwezi uliisha bila kuwasiliana na mtu yeyote, sikujua kilichokua kikiendelea kwa mume wangu wala ndugu zangu, sikua na simu, hakuna alityenitafuta na wala hakuna niliyemtafuta ingawa namba zao nilikua nazo.
Baada ya kama miezi miwili hivi ndiyo nilimpigia simu Mama yangu, nilimuambia kilichotokea na yeye akaniambia kuwa mume wangu ananitafuta nimetoroka na mtoto. Nilimuambia wala sijatoroka ila nimemuacha, kumbe mume wangu alishaenda mpaka na polisi, walikua wakinitafuta kana kwamba nimetoroka na mtoto. Mimi sikukimbia nilirudi nikakamatwa na polisi wakaniuliza kilichotokea niliwaambia kuwa nimetengana na mume wangu na naendelea na maisha yangu.
Mume wangu alikataa kuniacha na kusema kuwa anataka tuongea kashabdilika, nilimuambia kabisa kama kabadilika ni yeye mimi hainihusu, simatki na sitaki chochote kutoka kwake nina maisha yangu. Baada ya kuona kuwa nina msiamamo siwezi kurudi kwake aling’ang’ania mtoto, aliniambia kuwa kama naondoka basi nimuachie mtoto. Kwanza nilicheka lakini mwisho nikamuambia kuwa mtoto ni wakwake, mimi naweza kumhudumia lakini kama anamtaka ni ruhusa kumchukua, tududi polisi tuandikishane kuwa amelazimisha kumchukua mtoto wakati mimi nina uwezo wa kumlea.
Nilitaka tuandikishane kabisa kuwa mwanangu mimi sijamtelekeza bali ni Baba yake kamtaka na nina uwezo wa kumtembelea wakati wowote. Hilo nail alikataa nikamuambia basi kama anamtaka afuate sheria kuninyang’anya, nilijua kuwa lengo lake ni kunikomoa, alikua hahitaji mtoto, alitaka mimi niendelee kuishi kwake aninyanyase kisa mtoto. Nilikataa, ndugu waliingilia kati lakini sikuwajali. Aliniacha na mwanangu na kusema hatahusumia, nilimuambia kuwa mwanangu atakula ninachokula lakini sitarudi kwake hata nikiwa maiti.
Aligoma kutoa talaka akiwa haamini kabisa kuwa nimemuacha, nilifuatilia talaka BAKWATA wakagoma kunipa pia, nilimuambia kuwa talaka ni makaratasi lakini mimi nishakuacha, nilimpotezea kabisa na sikumtafuta, sikuhangaika wala nini, nimeendelea na Biashara ya nguo kwa mwaka sasa, nina duka langu la nguo, si kubwa sana lakini najihudumia mwenyewe. Napika maandazi asubuhi nauza, napika pia chakula kwenye sherehe, ndugu walinitenga ila sasa hivi naona wanajileta kwakua nina vipesapesa vyangu.
Mama mkwe kila siku ananipigia simu kuniambia kuwa mimi ndiyo mke anayenitambua nirudiane na mwanae kwani kawa mlevi kila siku ni mwanamke mpya haeleweki pesa haionekani. Nimemuambia Mama huyo ni mwanao pambana naye mimi hanihusi, si kazi yangu kumbadilisha na si kazi yangu kuvumilia, nina maisha yangu na wala hanihusu. Siko wkenye mahusiano kwakua sijaamua lakini si kwakua ndoa hainiruhusu, hapana nimeamua kuachana naye na sirudi nyuma, nimeandika kisa changu baada ya kusoma kisa cha David na kusoma Comment za watu.
Kuna wanawake wengi wanatukana na kuuliza mtu utavumiliaje yote hayo, mimi nimevumilia mengi zaidi ya hayo. Iko hivi mwanamke kama huna kazi mwanaume anaweza kukufanya chochote, wengi tunaishia kusema naondoka nina kwetu, ila huko unakokuita kwenu watakuchoka na utarudi kwa mwanaume yuleyule kwakua tu una njaa. Wanawake wengi ni waoga wa kuanza na mara kahdaa tunasema atabaidlika lakini hawabadiliki, hivyo kama unateseka badala ya kuhangaika kumbadilisha basi badilika wewe, tafuta kazi na acha kuwa tegemezi wa kila kitu.
***MWISHO

0 Comments