
Mara nyingi michango ya wanawake katika sekta muhimu kama
Teknolojia na sayansi haionekani lakini historia inaonesha jinsi gani wanawake
walivyotoa mchango mkubwa hasa katika karne ya mapinduzi ya viwanda.
Leo nimeona nikuletee hii listi ya wanawake waliotoa mchango mkubwa katika
kufanya vumbuzi mbalimbali za kisayansi duniani.
1:Florence Parpart.
Mwaka 1914 Florence Parpart alivumbua friji la kisasa linalotumia umeme ambapo
uvumbuzi huo uliweka rekodi ya dunia baada ya kuvumbuliwa na mwanamke.
2:Marie Van Brittan.
Anajulikana zaidi kwa mchango wake mkubwa katika uvumbuzi wa kamera ya cctv
mwaka 1969,ambapo ugunduzi huu aliufanya baada ya kukithiri kwa uhalifu katika
jiji la Newyork.
3: Stephanie Kwolek .
Stephanie Kwolek atakumbukwa kwa uvumbuzi wake wa material iliyotumika
kutengeneza bullet proof.
4:Hedy Lamarr’s .
Ni mwafizikia aliyebobea katika maswala ya mawasiliano ambapo aligundua
teknolojia ya wireless iliyo saidia kuanzishwa kwa wiFi na mfumo wa GPS.
5:Josephene Cochrane.
Mwaka 1887 Josephene Cochrane alivumbua machine ya kuoshea vyombo au dish
washer ambazo alikua akiziuza mahotelini mwaka mmoja baadae alifungua kiwanda
chake.
6:Letitia Gee.
Mwaka 1899 Letitia Geer Alivumbua bomba la sindano na kubadilisha historia ya
sekta ya afya milele.
7: Dr Maria Telkes.
Dr Maria Telkes mwaka 1947 alijenga nyumba ya kwanza duniani yenye mfumo wa
umeme wa jua au solar energy.
8:Maria Beasely.
Mwaka 1886 Maria Beasely alibuni maboya ya kuogelea au life jackets baada ya
kukithiri vifo vya baharini , ni uvumbuzi uliopongezwa na watu wengi na
kumfanya Maria Beasely kua mwanasayansi mwenye jina kubwa.
9:Dr Shirley Jackson
Ni mwanafizikia aliebuni nyaya au fiber cable zinazotomika leo hii kwenye
mitandao ya simu, pia uvumbuzi wake mwingine ulio mjengea jina ni pamoja na
machine ya fax, mfumo wa kusubirisha mtu kwenye simu au call waiting.
10:Ada Lovelace.
Unaweza usiamini lakini computer programmer wa kwanza kabisa duniani ni
mwanamke ,Ada Lovelace alikua mtu wa kwanza kubuni program mbalimbali za
computer.

0 Comments