Header Ads Widget

Responsive Advertisement

FILAMU YA YESU YENYE REKODI ZA KIPEKEE

.com/-PnHjjEOBCf0/XDptkkK_YOI/AAAAAAAACu0/zLJ-3WtSrwAzw4O7pN9yoMyvWyg3ixrsACHMYCw/



 Hivi kwa mfano ukipewa nafasi ya kutaja ni filamu gani ambayo unahisi itakuwa imeangaliwa zaidi duniani, ni majina yapi na yapi yatakujia kichwani? 
    Je, ni majina kama Avatar yenye mauzo ya muda wote ya zaidi ya dola za kimarekani 2.7 billion ambayo ni zaidi ya mara 10 ya bajeti yake, au labda Titanic yenye mauzo ya jumla ya zaidi ya dola billion 2.2 za kimarekani? 

    List inaweza kuongezeka pengine kwa ingizo la filam kama AvengersThe lion KingStar wars na nyingine nyingi, lakini nikikuambia kuwa hamna hata mojawapo kati ya hizo filamu imeongoza kwa kuangaliwa zaidi, unaweza ukashtuka na kuanza kujiuliza itakuwa ni filamu gani basi iliyoongoza kuangaliwa kama si hizo filam maarufu za muda wote.

     Mwaka 1979, waongozaji wa filamu  John Krish na Peter Sykes, waliyaweka mawazo ya muandishi Barnet Bain katika vitendo na ndipo walipoona kuwa Brian Deacon anaweza kuwa mtu sahihi katika ukamilifu wa kuigiza kama Yesu katika filam iliyokwenda kwa jina la JESUS. Ndio filamu iliyoongoza kwa kuangaliwa na watu wengi zaidi duniani na hivyo kumfanya muigizaji Brian Deacon kuwa mcheza filamu aliyetazamwa na watu wengi zaidi. 
Katika moja ya interviews ama mahojiano yake, Deacon aliwahi kusema kuwa hapo mwanzo alikua akipata shida kidogo hata kutoka nje ya nyumba yake baada ya watu wengi kudhani kuwa ndie Yesu Kristo halisi na hivyo kumzonga katika mizunguko yake wakitaka awabariki. 
Tuachane na story ya Deacon kwanza, Offset itakuwekea story hiyo wakati mwingine, lakini kwa sasa turudi kwenye filamu ya 'JESUS'.

    Katika kile kilichoaminika kama ndo changamoto za hapa na pale katika kazi, filamu hii ilipotoka tu, ikala hasara ya dola za kimarekani millioni 2 taslim, na ikumbukwe kuwa kwa mwaka 1979 pesa hiyo ilikuwa ni nyingi sana (ofcourse ni nyingi hata kipindi hiki) lakini kwa kipindi kile ilikuwa ni hasara kubwa isiyoelezeka. 

     Ikaja kutokea kama bahati, pale ambapo shirika moja la masuala ya dini chini ya bwana Bill Bright ambao kimsingi ndio wamiliki wa project ya filamu ya 'JESUS' ilipoichukua filamu hiyo na kuitafsiri kutoka lugha ya kiingereza kwenda lugha mbalimbali za mataifa mengine kisha kuiweka katika mfumo wa mkanda wa video ama kwa jina maarufu, VHS, na kuigawa bure mikanda hiyo kwenda kwa mataifa mbalimbali. Mpaka wakati huu filamu hiyo imetafsiriwa katika lugha zaidi ya 1500.

   Kufikia mwaka 2004 gazeti la 'New york Times' lilitoa takwimu kuwa takriban watu billion 3 wameshatazama filamu hiyo na kulingana na mtandao maarufu wa takwimu duniani 'worldometer' mwaka 2004 dunia ilikua na wakazi billion 6, kwa hiyo kwa mahesabu ya haraka haraka, nusu ya wakazi wa dunia nzima walitazama filamu hiyo kufikia mwaka 2004, ni ajabu lakini ndo ukweli.
 
    Huenda masuala ya kiimani yalichangia filam hii kuangaliwa zaidi, au pia huenda ni umahiri tu wa Madirector John, Sykes na muandishi Bain bila kusahau kipaji cha Deacon, vyovyote ambavyo sababu inaweza kuwa, lakini 'JESUS' ndio imeshika namba moja katika list ya filamu zilizotazamwa zaidi.

Post a Comment

0 Comments